Habari za Mastaa

Baraka Da Prince kayatoa ya moyoni waliosema ameshindwa kuongea kiingereza

on

Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 aliingia kwenye headlines baada ya mpenzi wake Najma kuonekana kuwa kama mkalimani wake kwenye interview ya MTV Base.

Sasa leo August 21, 2016 millardayo.com & Ayo TV aliimpata Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni>> Unajua watanzania asilimia kubwa wanakuwa wanakurupuka sana mimi sijaona kwanza kitu cha ajabu cha mimi kutumia lugha ya Kiswahili, mimi nimeenda MTV Base nimeulizwa Je unataka kutumia lugha gani ili uwe huru nikawajibu ninaweza nikatumia lugha ya Kiingereza lakini sitokuwa huru’

‘Sasa wabongo walifurahi wengine wakasema nimeshindwa kuongea kingereza kwangu mimi nimeitangaza  lugha yangu ya kiswahili halafu Najma hakuwa mkalimani wangu mimi bali alikuwa anawambia yule mtangazaji kile ninachokizungumza mimi’- Baraka Da Prince

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Baraka Da Prince akitoa ya moyoni kuhusu waliosema ameshindwa kuongea kingereza

ULIIKOSA MAJIBU YA EMMANUEL MBASHA KUHUSU KURUDIANA NA FLORA MBASHA BASI PLAY HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments