Premier Bet
TMDA Ad

Breaking News

BREAKING: Walioondolewa FIESTA 2017 Dar es salaam wamerudishwa

on

Ilitangazwa kwamba Tamasha kubwa la FIESTA 2017 Mkoa wa Dar es salaam litafanyika mpaka saa saba usiku ambapo taarifa hizo zikafanya kamati kuwaondoa Wasanii zaidi ya 15 kwenye orodha ya kutumbuiza sababu ya badiliko la muda wa kumaliza sherehe hii kubwa ya Taifa la Bongofleva.

BREAKING NEWS ambayo imetokea mchana huu kupitia XXL ya CloudsFM ni kwamba Wasanii wote walioondolewa wamerudishwa kwenye orodha na mipango yao ya kazi itaendelea kama kawa.

Swali kubwa ni Je kwasababu Wasanii hawa wamerudishwa kwenye orodha, FIESTA haitoisha tena saa saba usiku? kuna mpango wa FIESTA kukesha kama ilivyofanyika kwenye mikoa mingine??? endelea kusikiliza CloudsFM na kutembelea millardayo.com taarifa kamili utaipata baadae

Tayari kupunguzwa huko kwa muda kulishafanya baadhi ya Wasanii waondolewe kwenye orodha ya Wanaotumbuiza kwenye tamasha hilo akiwemo Lulu Diva, mtazame akiongea hapa chini

VIDEO: PAUL MAKONDA AFIKA CLOUDS NA KAMATI YA ULINZI, TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments