Habari za Mastaa

Huyu ndiye msanii mpya anaefuata kutoka Tetemesha 2014.

By

on

IMG-20140224-WA0008Tetemesha Records ni moja kati ya studio zilizoanzia safari yake ya kimuziki mikoani na kisha kuhamia Dar es salaam, awali makazi ya studio hii yalikua 88.1 Mwanza Kwa Dar es salaam rasmi ilihamia 2012 na kwa sasa Tetemesha inamtambulisha msanii wake mpya aitwaye Barakah da Prince.

Msemaji wa studio hiyo amesema kuwa Barakah ndiye atakua msanii mpya kwa mwaka 2014 kutoka Tetemesha ambaye anatarajiwa kutoa video mpya iliyotayarishwa na Director Nisher kutoka Arusha.

Barakah da Prince atakua ni msanii wa nne kutambulishwa na Tetemesha Records baada ya Hussein Machozi,Sajna na C-Sir Madini.

Video na audio za Barakah zinatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Tupia Comments