Top Stories

Burundi wanapiga kura kumuongezea Rais muhula

on

Leo May 17, 2018 Raia wa Burundi wnapiga kura ya maamuzi ya kuongeza muhula wa rais kutoka miaka tano hadi saba.

Marekebisho hayo ya katiba yakiidhinishwa na wananchi huenda rais Pierre Nkurunziza akaongoza taifa hilo hadi mwaka wa 2034.

Lakini kampeni hizo zimechafuliwa na tishio za upinzani kususia kura hiyo ya maamuzi huo na pia madai kwamba serikali imekuwa ikiwatisha wafuasi wa upinzani.

Umoja wa mataifa unahofia huenda ghasia zikazuka baada ya mauaji ya watu 26 hivi majuzi.

MAGAZETI LIVE: Ishu ya wanawake wenye Makalio, Nape Bashe waamsha Dude

 

Soma na hizi

Tupia Comments