Mix

Pale ambapo harufu ya choo cha ndege inafanya safari ikatishwe…

on

Runway

Ni kawaida kusikia kwamba ndege imeahirisha safari ama imekatisha safari kutokana na hitilafu ama dharura, ishu kama ya hali ya hewa ikiwa mbaya haishauriwi kuiacha ndege iendelee na safari hiyo.

Dharura iliyoikuta ndege ya shirika la ndege la British Airways na kulazimika kukatisha safari kutokana na harufu mbaya iliyokuwa ikitokea ndani ya choo hii ni story ambayo iko kitofauti kidogo.

Ndege hiyo ilikuwa imetoka Heathrow Uingereza kuelekea Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua kama saa saba.

Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo Abhishek Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa walilazimika kurudi kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow kutokana na tatizo la choo cha ndege hiyo kutoa harufu mbaya.

Abiria huyo alionekana kukasirishwa na kitendo cha safari yao kuahirishwa na kulazimika kurudi Uwanja huo wa ndege ambapo walikaa kwa saa 15 mpaka ilipopatikana ndege nyingine ya kuwasafirisha abiria hao kwenda Dubai.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments