Duniani

Utata ulivyoibuka baada ya watu wa Brazil kuzuiwa kutumia WhatsApp..

on

Mtandao wa WhatsApp umekamata sana sasahivi kutokana na watu wengi kupendelea kuutumia mtandao huo, inakuwaje una smartphone yako alafu unazuiwa kutumia WhatsApp ?!! Brazil imewakuta hiyo.

Ishu ilianza hivi, Mahakama ya Brazil iliagiza wamiliki wa mtandao huo kuwapa nafasi ya kuweza kuingilia na kupekua taarifa za kila mtumiaji wa mtandao wa WhatsApp aliyepo Brazil, lakini wamiliki hao hawakuwa tayari kuingia masuala ya mawasiliano ya mtu binafsi, wakapingana na maagizo hayo… agizo likatolewa na Mahakama kwamba mtandao huo ufungwe kwa saa 48, maana yake ni kwamba watu wote wa Brazil kwa jana hawakuwa na mawasiliano ya WhatsApp.

brazilian-court-puts-48-hours-ban-on-whatsapp

Lakini mbali ya watu wengi kukosoa uamuzi huo, Boss wa Facebook ambae ndiye mmiliki wa WhatsApp pia, Mark Zuckerberg alilaani kitendo hcho kwa kuandika haya >>> ‘Nashtushwa kwamba jitihada zetu kulinda siri za watu kunapelekea Jaji mmoja kuamua maamuzi haya mabaya kuadhibu kila mtu aliye ndani ya Brazil anayetumia WhatsApp‘- Mark Zuckerberg.
MARK

Lakini baadae, Zuckerberg alipost pia ujumbe kwenye ukurasa wake Facebook kushukuru baada ya watumiaji wa WhatsApp kurudishwa tena hewani Brazil.

MARK II

Uamuzi huo ulikuja baada ya Mahakama moja Brazil kuagiza mtandao wa WhasApp kutoa taarifa mbalimbali ili kusaidia kukamilisha wa kesi za jinai zilizokuwa Mahakamani, lakini wamiliki wa mtandao hawakuwa tayari pia kuruhusu taarifa hizo kutolewa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments