Habari za Mastaa

Kumbe Solange amefuta picha zake na Beyonce insta akaacha hii tu, tazama alichofanya Beyonce

on

Screen Shot 2014-05-15 at 6.10.44 AMKwa wale mnaofatilia stori za mastaa, ikiwa ni chini ya saa 48 toka iripotiwe kwamba Solange ameziondoa kwenye page yake ya instagram picha alizopiga na dada yake yaani Beyonce, B amejibu kwa kufanya maamuzi ya kuweka kumbukumbu za hizi picha nne alizopiga na Solange.

Mwanzoni ilionekana ugomvi ni kwa Solange na Jay Z ila kuna kitu kinaendelea manake uamuzi wa Solange kufuta picha za Beyonce kwenye insta yake umekuja baada kusambaa kwa video ikimuonyesha yeye (Solange) akimpiga Jay Z kwenye lift ya hoteli huku Beyonce akiwa pembeni akishuhudia bila kuingilia kati hata kwa kumzuia Solange.

Screen Shot 2014-05-15 at 6.25.45 AM

Screen Shot 2014-05-15 at 6.34.29 AM

Hii ndio picha pekee Solange aliyokua kaibakiza kwenye instagram yake lakini sasa hivi haionekani na kuna uwezekano ameshaifuta tayari.

Saa kadhaa baada ya picha zake kufutwa na Solange, Beyonce alipost picha 4 akiwa na Solange ndani ya saa 17 huku moja tu ndio ikiwa na caption ya ‘good morning’ ila nyingine hajaandika kitu.

Screen Shot 2014-05-15 at 6.30.27 AMImeripotiwa kwamba hakuna maelewano mazuri kati ya ndugu hawa wawili Beyonce na mdogo wake Solange.

Screen Shot 2014-05-15 at 6.30.41 AM

‘Good morning’

Screen Shot 2014-05-15 at 6.37.22 AM

Baada ya Solange kuonekana akimpiga Jay Z kwenye lift zilitoka stori za chinichini kwamba Rihanna ndio chanzo cha yote ambapo Beyonce amezikanusha hizo stori kwa kuweka picha akiwa na Rihanna kuonyesha kwamba kila kitu kiko poa.

Kaa karibu na mimi kupitia Twitter kwa kubonyeza HAPA, pia Instagram na Facebook kwa kubonyeza INSTA na FB ili kila stori inayonifikia niitume kwako iwe usiku au mchana.

Soma na hizi

Tupia Comments