AyoTV

VIDEO: ‘Ni halali wananchi kulipa ushuru wakati hawapati huduma?’-Mbunge Hussein Bashe

on

Headline kutoka bungeni Dodoma June 02 2016 kazi ilikuwa ni maswali na majibu kutoka kwa wabunge kuielekezea Serikali, kazi ya ufafanuzi ilikuwa ikitolewa na Mawaziri. Wabunge mbalimbali waliipata nafasi hiyo ya kuwasilisha maswali yao, lakini hii ya Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe yeye alisimama kutoa taafifa rasmi.

Hapa anasema…>>’Leo saa tisa usiku katika soko kuu la wilaya ya Nzega kumetokea moto mkubwa ulioteketeza baadhi ya maduka ya wafanya biashara, lakini hoja yangu ni kwamba kwa miaka mitano wamekuwa wakilipa ushuru wa zima moto na taasisi hii imeshindwa kuwapatia huduma wananchi.

Sasa nataka tujadili kwa pamoja pale ambapo mwananchi anatimiza wajibu wake wa kidheria wa kulipia huduma kwenye taasisi na taasisi hiyo inashindwa kumpatia mwananchi huduma. Je, ni halali wananchi kuendelea kulipa ushuru wakati hawapewi huduma stahiki

ULIIKOSA HII? MAOMBI YA MBUNGE INNOCENT BASHUNGWA KWA WAZIRI BUNGENI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments