Bongo Star Search imerudi tena mtu wa nguvu, huu ni msimu wa nane wa mashindano hayo tangu yameanza… mikoani kazi imeisha na washiriki wamepatikana, sasa ni zamu ya Dar es Salaam.
Baada ya Majaji kuwakusanya washiriki waliofanya vizuri Mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya sasa kazi imeanza rasmi Dar es Salaam ambapo usaili ulianza July 22 2015 na utaendelea mpaka July 24, mchakato wote unaendelea pale Coco Beach.
Kama kawaida majaji wa mashindano haya ni Madam Rita, Master J na Salama Jabir… kazi yao kubwa ni kuwachuja wale wote wanaojitokeza kwenye usaili huu na hatimaye kuwapata wale bora zaidi watakaoiwakilisha Dar es salaam kwenye fainali msimu huu.
Kazi ilikuwa kubwa kwa siku ya leo Coco Beach, watu wameonesha kupania kufanya kweli safari hii… walijitokeza kwa siku ya leo tu ni watu wengi sana na siku ikaisha kila kitu kikaenda vizuri.
Hapa chini nimekusogezea picha zikionyesha leo palivyokuwa Coco Beach.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.