Habari za Mastaa

Rich Mavoko “Sikufanya fujo nyumbani kwa Lulu Diva, Ila fresh amenilipa” (+Audio)

on

Leo May 29,2019 Msanii wa Bongo Fleva Rich Mavoko ameachia rasmi ngoma yake ‘Usizuge’ ikiwa ameitambulisha kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM na kufanya mahojiano kuhusu vitu mbalimbali ikiwemo na ishu ya kumvamia Lulu Diva nyumbani kwake kudai hela yake.

“Kiukweli sikwenda kufanya fujo nyumbani kwa Lulu Diva ila tu alipitisha muda wa malipo..tulipatana muda fulani akapitiliza ila fresh Lulu ameshanilipa” alisema Rich Mavoko baada ya kuulizwa swali kuhusu Lulu Diva ikiwa  wawili hao walishawahi kufanya kazi pamoja kwenye ngoma ya ‘Ona’.

Rich Mavoko aligusiwa pia kuhusu kurudi kufanya kazi kwenye Management aliyokuwepo awali na alisema “hakuna kitu kama hicho na kuonegeza kwamba ,Ni heri kubakia na nguo iliyochanika kuliko kubakia tumbo wazi”

VIDEO: ULIPITWA NA HII KWA MARA YA KWANZA JACQUELINE AANDIKA KUMHUSU MUMEWE DR. MENGI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments