AyoTV

Azam FC kugawa Ice Cream Bure Chamazi ili kuvuta mashabiki vs Fasil Kinema

on

Club ya Azam FC kuelekea mchezo wake wa marudiano wa Kombe la shirikisho Afrika, imetangaza kuwa kila shabiki atakayekata tiketi ya kuingia uwanjani Chamazi siku ya Jumamosi ya August 24 2019 dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia atapewa Ice Cream ya Ukwaju bure.

Azam FC ilipoteza mchezo wa kwanza nchini Ethiopia kwa goli 1-0,  hivyo Jumamosi inaingia uwanjani ikiwa na tahadhari ya kutaka kupata ushindi huku ikiepuka kuruhusu goli la mapema, kwani ikitokea wameruhusu hivyo utakuwa ni mlima kwao.

Ushindi wa kuanzia 2-0 unaweza kuivusha Azam FC katika hatua inayofuatia ya michuano ya Kombe la shirikisho Afrika, wapinzani wa Azam FC tayari wamewasili na walifikia maeneo ya Vingunguti na wamekuwa wakiutumia uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi.

VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu

Soma na hizi

Tupia Comments