Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliripoti katika Kituo cha Polisi, Kamata Dar es Salaam kutekeleza wito kama alivyotakiwa awali na Jeshi hilo kwa ajili ya kuhojiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu-Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu, amesema baada ya kumhoji, Polisi wamechukua simu yake kwa maelezo kuwa itasaidia katika uchunguzi wao na kuahidi watairudisha kwake kesho jioni huku wakimtaka arudi tena kituoni hapo November 21, 2017.
Aisha, Ado amesema, Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo kufanya upekuzi wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi “UNASINYAA”.
ZITTO: ‘Sisi sio Mawakala wa Polisi, hawana mamlaka kuhoji Kamati Kuu”