Premier Bet
TMDA Ad

Mix

PICHA 7: Bugatti kutengeneza baiskeli itakayouzwa Tsh milioni 85

on

Kampuni ya kutengeneza magari ya Bugatti ya Ufaransa imetangaza kutengeneza baiskeli za kisasa ikishirikiana na kampuni ya kutengeneza baiskeli ya PG.

Bugatti itatengeneza baiskeli hizo ambazo zitakuwa nyepesi zaidi zikiwa na uzito wa 5 kg zitakazotumika kwa ajili ya michezo lakini zitakuwa na gharama kubwa zikiitwa PG Bugatti Bike ambapo unaambiwa licha ya kuwa na uzito mdogo baiskeli moja itagharimu $39,000 (£32,000) ambazo ni zaidi ya Tsh. milioni 85 .

Bugatti inatarajia kuziachia modeli 667 zikiwa na rangi tofauti baadaye mwaka huu na hazitotumika kwenye barabara za umma.

Nimekuwekea hapa picha za muonekano wa baikeli hiyo.

VIDEO: Air Tanzania yakusanya BILIONI 9 kwa miezi minne. Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments