Habari za Mastaa

VIDEO: “Watu waliotaka kuniroga walinipigia simu tena”

on

Kipindi cha Nyuma msanii wa muziki wa Asili Saida Karoli alishawahi kuzungumza na Ayo Tv kuhusu watu waliomtishia maisha kwa kumpigia simu na kumwambia walitaka kumpoteza, sasa Ayo Tv ilimpata Saida Karoli Kahama ambapo alikuwa akitoa burudani kwenye jukwaa la Fiesta mjini humo.

Saida amezungumzia ishu hiyo ambapo alisema kuwa watu wale hawakuishia pale kwani walimpigia tena simu na akazungumza nao lakini mara hii waliahidi kutomdhuru tena kwani hapo mwanzo waliagizwa tu kumtishia lakini ukweli ni kwamba wenyewe wanapenda na kumtakia kila la kheri.

Msikilize Saida Karoli akielezea kila kitu kwa kubonyeza PLAY hapa chini..

Chege kaulizwa, ana mpango wa kumuoa aliyempost Instagram?

Soma na hizi

Tupia Comments