fB insta twitter

Utafiti umefanyika wanaotaka Bunge ‘live’

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya stori ambayo imeandikwa June 16 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘watu 9 kati ya 10 wataka Bunge ‘live’

Gazeti limeripoti utafiti uliofanywa na shirika la Twaweza ambapo umebainisha kwamba watu wanane kati ya kumi sawa na asilimia 79 ya waliohojiwa, wanapinga uamuzi wa Serikali kusitisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya mijadala ya Bunge.

Gazeti hilo pia limeeleza kwamba katika utafiti huo watu tisa kati ya kumi, sawa na asilimia 92 wanataka Bunge live, utafiti huo uliofanywa  kati ya March 29 na April 12 kupitia mpango wa sauti za wananchi na kutangazwa jana, matokeo yanaonyesha wananchi wanapinga hatua hiyo wakidai ni haki yao ya msingi kujua kinachoendelea Bungeni.

Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo 

ULIKOSA KUTAZAMA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNI 16 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments