Top Stories

Nimeyapata matokeo ya Uchaguzi wa Wagombea Ubunge wa CCM Jimbo la January Makamba Bumbuli

on

printHeadlines za sasa nyingi zimeelekea kwenye siasa ambapo Tanzania mwezi October 2015 itakua ni muda wa Watanzania wote kuwapigia kura wagombea ambao wanaona wanafaa.

Yamenifikia matokeo ya uchaguzi wa Wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi jimbo la Bumbuli, ambazo zimetolewa na Ramadhan Mahanyu Mkurugenzi wa Uchaguzi wilaya ya Lushoto.

bumbuliJanuary Yusuph Makamba amepata kura 17,805 alafu mgombea mwingine ni Abdulkadir Abdi Mgheni yeye amepata kura 2,403, Abubakar Juma Mshihiri yeye amepata kura 205 na Yusuph Juma Shekwavi amepata kura 69.

Nimeambiwa pia kura zilizopigwa ni 20,522 kati ya hizo 40 ziliharibika na 20,482 ni kura halali.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments