Michezo

Nimekuwekea matokeo ya Borussia Dortmund VS Bayern Munich mtu wangu

on

Wikiendi mbili zilizopita tulishuhudia vilabu mahasimu wa ligi za England Manchester UTD vs Liverpool na FC Barcelona vs Real Madrid wakiumana.. leo ilikuwa zamu ya wababe wengine tena Bundesliga ambapo Borussia Dortmund waliwakaribisha wapinzani wao Bayern Munich katika dimba la Siguna Iduna Park.

Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita umeshuhudia Bayern wakipata ushindi mgumu wa goli 1-0 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.

Robert Lewandoski mchezaji wa zamani wa Dortmund ndio aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa timu yake ya zamani baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliokolewa na kipa wa Dortmund mapema katika kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Bayern Munich wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani.

Matokeo mengine ya Bundesliga unaweza kucheki hapa..

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments