Uwezekano wa kurejea kwa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) inawezekana ukawa mashakani baada ya club ya Cologne kubaini wagonjwa watatu wa corona.
Alhamisi ya wiki hii club hiyo iliwafanyia vipimo wachezaji, viongozi na benchi zima la ufundi na kubaini kuwa watatu kati yao wana corona.
Cologne wamekataa kuwatangaza au kutaja nafasi zao katika timu sababu ya kuweka privacy, hata hivyo club hiyo imesema club itaendelea na mazoezi kwa makundi kama kawaida, vilabu vya Bundesliga vilianza mazoezi toka April 6.