AyoTV

VIDEO: Imenifikia hii ya kuhusu Mipaka ya Wafugaji na Wakulima Tanzania

on

Bunge la 11 limeendelea tena Dodoma leo Mei 5 2016, Katika Kipindi cha Maswali ya papo kwa pako kwa Waziri Mkuu Mbunge Sikonge Joseph kakunda amemuuliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa..>>>

Kumekuwa na migogoro ya Wakulima na wafugaji kugombea maeneo nchini, katika ilani ya uchaguzi kuna maelekezo kwamba Serikali itapima maeneo mapya, Je, ni lini Serikali hii kazi itatekelezeka?

Waziri Majaliwa akijibu kwa kusema.. >>’Nikiri kwamba sasahivi tuna migogoro mingi sana ya wafugaji na wakulima lakini pia migogoro ya jamii na jamii, Jambo ambalo amelieleza Mbunge ni miongoni ya mikakati tuliyonayo pia

Tumeanza kutafuta njia sahihi ya kuondoa migogoro ya ardhi, lakini wakati mwingine ni kutokana na utendaji wa hovyo wa watendaji wetu wa Serikali tuliowapa dhamana

Tunao wawekezaji wanaoingia kinyemela kwenye maeneo yetu na kujichukulia maeneo na kusababisha migogoro, Kwanza tumezipa maagizo Wizara zote husika watupe maeneo ya mipaka

Unaweza kuipata full stori kwenye hii video hapa chini…

ILIKUPITA HII WABUNGE WANAWAKE WAMJIA JUU WAZIRI KIGWANGALLA BAADA YA MAJIBU HAYA..?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments