Bunge la Kenya limepokea ombi la TikTok kupigwa marufuku nchini humo hii ni baada ya Wadau hao kusema jukwaa hilo linaongoza kwa uvunjaji wa kanuni ya faragha na kusambaza maudhui ya ngono.
Spika wa Bunge la Kenya, Moses Wetang’ula amesema ombi hilo limewasilishwa na Mwanaume aitwaye Bob Ndolo akidai TikTok inakusanya taarifa muhimu kutoka kwa Watumiaji wake, ikiwa ni pamoja na eneo na historia ya kufanya starehe na amesema jukwaa hilo linahamasisha vurugu, lugha chafu, kusambaza maudhui ya ngono na matamshi ya chuki.
TikTok yenye Makao makuu nchini China imelalamikiwa pia kuwa ina-share taarifa za Watumiaji na makampuni ya Wahusika wengine bila idhini yao, hata hivyo Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah amepinga marufuku ya TikTok na akiomba aliyetoa taarifa kuzingatia udhibiti wa programu hiyo.
Mnamo Aug 02, 2023 Serikali ya Kenya ilisema itapitia sheria za mtandao ili kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja wa mtandao wa TikTok usiku ambapo Watumiaji wanadaiwa kupeperusha maudhui yenye lugha chafu, Kenya ni miongoni mwa Nchi zinazoongoza kwa matumizi ya TikTok Ulimwenguni.