Bunge limeahirisha mjadala wa Wizara ya Afya ili kujadili sakata la malori kutoshusha wala kupakia mizigo katika bandari ya DSM.
Hoja ya kuahirishwa imewasilishwa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi, baada ya hoja hiyo Naibu Spika, Tulia Ackson aliruhusu hoja ijadiliwe kwa dakika 20 ambapo baadhi ya wabunge walipata nafasi ya kuchangia na baada ya michango hiyo upande wa Serikali ulipata nafasi ya kujibu hoja za wabunge ambapo Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekwenda DSM kushughulikia suala hilo.