Wabunge Nchini Somalia wamepiga kura kufuta nyongeza ya miaka miwili madarakani kwa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed iliyoidhinishwa mwezi Aprili baada ya jambo hilo kuibua mvutano mkubwa.
Mgogoro wa kisiasa umeibua wasiwasi kuwa Waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama ikiwa Vikosi vya Serikali vitagawanyika.
Watu 60,000 hadi 100,000 walilazimika kukimbia makazi yao kufuatia mapigano ambayo yalichochea hofu ya vita kati ya vikundi vinavyomuunga mkono Rais na vinavyompinga.