Habari za Mastaa

Pichaz za wasanii wakiwa ‘Mjengoni’ kwenye Bunge la Katiba.

on

20140218_194628Bunge la Katiba bado linaendelea 104.4 Dodoma na miongoni mwa watu waliopata fursa ya kuwepo kwenye bunge hili ni wasanii wa Tanzania ambapo jumla ya wasanii 12 wakiwa pamoja na viongozi toka Shirikisho la muziki,Shirikisho la Filamu,Shirikisho la Sanaa za ufundi na Mtandao wa Wanamuziki Tanzania hawa ni miongoni mwao waliowawakilisha wenzao Dodoma.

IMG_0052Sababu kubwa ya wasanii hao kuelekea Dodoma na kuwepo kwenye mfululizo wa mikutano na wabunge mbalimbali ni kuwashawishi wabunge waunge mkono vipengele viwili ambavyo wasanii wanavitaka katika Katiba

Vipengle wanavyohitaji wasanii ni pamoja na

  1. Kundi la wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa.
  2. Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote lililokutana nao.

IMG_0069

IMG_0070

IMG_0087

IMG-20140218-WA0037

IMG-20140218-WA0036

IMG-20140218-WA0050

IMG-20140218-WA0051

Picha:Mzee kitime.

 

 

Tupia Comments