Kambi ya upinzani bungeni imewashutumu Wabunge wa chama cha mapinduzi (CCM) kwamba wamehongwa mamilioni ya fedha (milioni 10 kila Mbunge) ili kupitisha muswada wa huduma za habari unaobishaniwa.
VIA Azam TV: Muswada huo umepangwa kufikishwa bungeni November 4 2016 ambapo madai hayo ndio yalimkwamisha asubuhi kiongozi Freeman Mbowe kumuuliza swali Waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya Naibu Spika kusema swali hilo halikua la kisera.
Kwenye mkutano na Waandishi wa habari baada ya hapo, Mbowe amesema ‘hizi fedha zinazogawiwa Bilioni 2.7 kila Mbunge amepewa burungutu la milioni 10 kwenye bahasha ya kaki na wamesaini pale makao makuu ya CCM, na watake tutoe ushahidi tutatoa ushahidi‘
Kufahamu mengine zaidi yaliyosemwa na Freeman Mbowe unaweza kubonyeza play kutazama kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Naibu spika vs Freeman Mbowe bungeni baada ya Mbowe kumuuliza Waziri mkuu swali la Wabunge wa CCM kupewa milioni 10.