Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wameagiza kusitishwa usambazaji wa jarida linalochapishwa kwa lugha ya Kifaransa la “Jeune Afrique” likituhumiwa kuwa limekuwa likijaribu kushusha hadhi ya jeshi la nchi hiyo.
Serikali ya Burkina Faso imekosoa makala mpya na ya kupotosha iliyochapishwa jana na jarida hilo la lugha ya Kifaransa chini ya anwani “Mvutano unaendelea katika jeshi la Burkina Faso”.
Makala hiyo tajwa inafuatia ile ya huko nyuma iliyochapishwa na jarida hilo la lugha ya Kifaransa katika tovuti moja Alhamisi iliyopita. Jarida la Jeune Afrique lilidai kuwa malalamiko yanazidi kuongezeka katika kambi za jeshi nchini Burkina Faso.
Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wameeleza katika taarifa yao wakijibu hatua ya jarida la Jeune Afrique kuwa:
“Madai haya ya kimakusudi yaliyotolewa bila uthibitisho hayana lengo jingine ghairi ya kulifanyia dharau jeshi la taifa.