Wizara ya afya nchini Burundi imethibitisha visa 171 vya maambukizo ya mpox, taarifa inayokuja baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa mwezi uliopita.
Zamani ukijulikana kama monkeypox, mpox ni ugonjwa unaambukizwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama ambapo pia unasambazwa baina ya binadamu kupitia kutagusana na mtu aliyeambukizwa.
Akithibitisha visa hivyo, waziri wa afya Polycarpe Ndayikeza aidha ameeleza kwamba hakuna mgonjwa aliyefariki kutokana na mpox.
Visa vitatu vya mpox vilithibitishwa jijini Burundi mwezi Julai mwaka huu, wizara ya afya ikiripoti maambukizo 153 tarehe 18 ya mwezi Agosti.
Afisa kwenye taifa hilo ameiambia AFP kwamba visa vilivyothibitishwa vinahusishwa na aina mpya ya vinavyoripotiwa katika nchi jirani ya DRC.
Licha kwamba mpox imekuwepo kwa miongo kadhaa, aina hii mpya maarufu kama Clade 1b imeonekana kuripotiwa kuongezeka katika siku za hivi karibuni.