Top Stories

“Busara itumike kesi ya Mbowe” Viongozi wa dini

on

Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Viongozi wa Dini mbalimbali ambapo wamejadili masuala ya maendeleo ya Nchi katika kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa masuala waliyozungumza ni elimu ambapo Viongozi hao wamependekeza kuwepo na mjadala mpana kuhusu mfumo mpya utakaokidhi mahitaji ya sasa kwa maana ya kutozalisha Jamii ya Wahitimu walioandaliwa kuajiriwa peke yake.

Wakati huohuo Viongozi hao wa Dini wametumia Mkutano wao na Rais Samia kuomba Mamlaka husika kutumia busara ili kuangalia namna ya kumaliza kesi inayomkabili Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Wenzake.

Soma na hizi

Tupia Comments