Habari za Mastaa

Busta Ryhmes matatani ajikuta mikononi mwa polisi…!!

on

busta3

Msanii wa Hiphop Marekani mwenye style yake ya kipekee kabisa ya ku-rap Busta Rhymes anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani.

Siku chache zilizopita msanii huyu alikuwa Gym moja iitwayo Steel Gym maeneo ya Chelsea jijini New York na wakati akiwa mazoezini msanii huyo aliingia kwenye majibishano na mtu mwengine kwenye Gym hiyo.

busta

Mabishano yakasababisha ugomvi mkubwa kati ya wawili hao, Busta Rhymes akapandwa na hasira na kumrushia mwenzake chupa…mwanaume huyo alieumia alikataa kupewa huduma ya kwanza na Gym hiyo bali akaamua kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha polisi na kufungua mashitaka ya ushambuliaji dhidi ya Busta Rhymes.

NEW YORK, NY - JANUARY 17:  Busta Rhymes  performs at VH1 Save The Music Foundation's Songwriters Music Series Remix featuring Swizz Beatz & Friends, presented by Monster DNA Headphones & William Hill Estate Winery at Hard Rock Cafe New York on January 17, 2013 in New York City.  (Photo by Bryan Bedder/Getty Images for VH1 Save The Music)

Mwanasheria wa Busta Rhymes amesema kitendo hicho ni cha kijinga kwani ugomvi aliuanzisha yeye na sio Busta kitendo cha kumshitaki ni nia mbaya ya kulichafua jina la msanii huyo… kwa sasa Busta Rhymes anashikiliwa na kituo cha polisi kwa mashitaka hayo.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments