Top Stories

Siku 7 zimetimia! Mahakama yampa onyo Wema Sepetu (+Picha)

on

Hatimaye leo June 24,2019 msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amerudishiwa dhamana yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota gerezani kwa siku 7 kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imemuonya msanii huyo endapo akirudia kukiuka masharti ya dhamana haitasita kumfutia kabisa dhamana hiyo.

Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kuchapisha picha za Ngono katika mtandao wa kijamii alifutiwa dhamana yake Juni 17, mwaka huu baada ya kushindwa kufika mahakamani hapo kwa siku mbili. Kesi imeahirishwa hadi Julai 4, 2019.

VIDEO: SIKU 7 ZA WEMA SEPETU GEREZANI, AUNT EZEKIEL AIBUKIA MAHAKAMANI

Soma na hizi

Tupia Comments