Habari za Mastaa

Taarifa mpya kuhusu Nicki Minaj kutokuwepo kwenye ziara ya Chris Brown

on

Baada ya kusambaa kwa taarifa za rapper Nicki Minaj kutokuwepo kwenye list ya majina ya wasanii watakaotumbuiza na mkali wa RnB Chris Brown kwenye ziara yake ya muziki “IndiGOAT” inayotangazwa kuanza hivi karibuni.

Sasa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Nicki Minaj hakuwahi kusaini mkataba wa kufanya ziara na Chris Brown na kuelezwa kuwa ndio maana hajatokea kwenye list hiyo japo waliwahi kujadili kufanya kitu kama hicho baada ya wimbo wao wa ‘Wobble Up’ kufanya vizuri na kufikisha watazamaji Mil.22 tokea uachiwe kwenye mtandao wa YouTube May 20,2019.

Chris Brown alitaja list ya wasanii watakaomsindikiza kwenye ziara yake kupitia ukurasa wake wa Twitter huku list hiyo inawakutanisha wakali kama Torylanes, Tydollasign, JoynerLucas na Yella Beezy.

VIDEO: UMEPITWA NA HAYA MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUMHUSU IDI AMIN UTABAKI MDOMO WAZI! BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments