Michezo

EPL imeanza MO Salah kama kawaida yake na game za ufunguzi

on

Ligi Kuu ya England msimu wa 2019/2020 imeanza rasmi leo Ijumaa ya August 9 kwa mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Norwich City ukichezwa katika uwanja wa Anfield, game hiyo imechezwa na Liverpool ambao ndio Mabingwa wa Ulaya wameanza msimu kwa kudhiirisha ubora wao.

Liverpool imeanza msimu kwa ushindi mnono wa magoli 4-1, magoli ya Liverpool yakipatikana dakika ya kwa Norwich kujifunga kupitia kwa Hanley, Mohammed Salah dakika ya 19, Van Dijk dakika ya 28 na Divock Origi akafunga goli la nne dakika ya 42 kabla ya dakika ya 64 Pukki kufunga goli la kufuatia machozi kwa Norwich.

Ushindi huo umeanza kwa kuipa baraka Liverpool ya kuwa timu ya kwanza kuanza kukaa kileleni mwa msimamo wa EPL kabla ya timu nyingine 18 kuchezwa, msimu uliopita Liverpool walipoteza nafasi ya kutwaa Ubingwa kwa tofauti ya alama chache sana dhidi ya Man City lakini msimu huu inawezekana wametia nguvu zaidi ya kuhakikisha wanaondoa ukame wa miaka zaidi ya 20 bila taji la EPL.

KOCHA ZAHERA KIKOSI KAMILI KAWEKA NJE KINAISUBIRI TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments