Top Stories

Baada ya kuonana na JPM, Rais wa JICA leo kawatembelea TANESCO

on

Jana August 21 2017 Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan ‘JICA, Shinichi Kitaoka, Ikulu Dar es Salaam.

Rais huyo wa JICA leo August 22, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alitembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme Ilala, DSM kilichojengwa kwa msaada wa Shirika hilo kwa Dola Milioni 38 kusaidia upatikanaji na usambazaji wa umeme.

Baada ya kufika katika Kituo hicho Shinichi alisema:>>>”Tanzania inakuwa kwa kasi kiuchumi na suala la kufanya nchi kuelekea katika uchumi wa viwanda kuna uhitaji mkubwa wa umeme ndio maana tumetembelea mtambo huu ili kuona jinsi unavyofanya kazi na kuona jinsi tutakavyoendelea kushirikiana.”

Serikali kuanza mchakato kusambaza gesi majumbani…play kwenye hii video kutazama!!

Soma na hizi

Tupia Comments