Duniani

Ni Dereva Tax alafu unagundua abiria wako muuza dawa za kulevya… ungefanya kama huyu?

on

Biashara ya Dawa za Kulevya inapigwa vita sana lakini ni uzalendo na ujasiri wa aina yake sana kujitolea kumkamata muuzaji wa dawa za kulevya mpaka unahakikisha anafika katika mikono ya Polisi.

Tumeona athari nyingi sana zinazotokana na watu kujiingiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, kama kila mtu angekuwa na moyo  wa huyu dereva wa Taxi, tatizo lingepungua sanaaa.

Story kutoka Manispaa ya Chongqing nchini China iliyogusa kwenye vichwa vya habari ilihusu kitendo cha kijasiri kilichofanywa na dereva wa Taxi ambaye aliamua kumpeleka abiria wake moja kwa moja Kituo cha Polisi baada ya kumhisi kuwa jamaa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya !!

Baada ya Dereva kusimamisha Taxi yake kituo cha Polisi, abiria wake alichomoka na kuanza kukimbia huku akiutupa mzigo wa Begi lake nyuma… hakufika mbali, Polisi wakashirikiana na Dereva kumkimbiza mpaka kumkamata.

Dereva wa Taxi kumbe hakukosea, ndani ya Begi kumekutwa Dawa za Kulevya zenye uzito wa Kilo moja pamoja na visu kadhaa, tayari Mtuhumiwa yuko mikononi mwa Polisi na ana Kesi ya kujibu,  mwanzo mwisho wa tukio lenyewe lilinaswa na camera ya CCTV…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments