Michezo

CAF wairuhusu Simba SC kuingiza mashabiki vs AS Vita

on

Shirikisho la soka Afrika CAF kupitia TFF limeruhusu mchezo wa Simba SC dhidi ya AS Vita wa Ligi ya Mabingwa Afrika April 3 2021 kuingizwa mashabiki 10,000.

Awali CAF walizuia Simba SC kucheza na mashabiki katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya El Merreikh ya Sudan uliyochezwa Uwanja wa Mkapa kwa sababu ya kujikinga na Corona.

Kwenye mchezo huo uliochezwa March 16 2021 uwanja wa Mkapa na Simba kupata ushindi wa magoli 3-0, Simba waliruhusiwa kuingiza watu 200.

Soma na hizi

Tupia Comments