Shirikisho la soka Afrika (CAF) leo limechezesha droo ya kupanga Makundi ya michuano ya CHAN 2024 ambapo Tanzania imepangwa Kundi B na timu za Madagascar, Mauritania, Afrika ya Kati na Burkinafaso.
Michuano ya CHAN 2024 inachezwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Uganda na Kenya na sasa imeahirishwa kutoka kuchezwa February mwaka huu hadi August 2025 kwa sababu ya kutoa muda zaidi wa maandalizi kwa mataifa wenyeji.