Michezo

CAF imechezesha droo ya CHAN 2018, watakaocheza na Tanzania wametajwa

on

Shirikisho la soka barani CAF leo Fabruary 3 2017 Libreville Gabon limechezesha droo ya kupanga timu zitakazoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika 2018 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani maarufu kama CHAN 2018.

Droo hiyo imechezeshwa na kwa upande wa timu ya taifa ya Tanzania katika haraka za kuwania kucheza michuano hiyo, imepangwa kuchezwa na Rwanda round ya pili, mchezo ambao utachezwa  kati ya July 14 na 16  Dar es Salaam kabla ya kurudiana tena kati ya July 21 na 23 Kigali Rwanda.

Kamati ya CAF ambayo imechezesha droo hiyo ikiwa Libreville Gabon imepanga nchi hizo za ukanda wa Afrika Mashariki na kati, kuwa mshindi kati ya Rwanda na Tanzania atakutana na mshindi kati ya Uganda, Sudan Kusini na Somalia.

Mara ya mwisho kwa timu za taifa za Rwanda na Tanzania kukutana ilikuwa katika michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2015 Ethiopia, lakini Rwanda ilipoteza kwa goli 2-1 kabla ya kumaliza michuano hiyo kwa Rwanda kushika nafasi ya pili kwa kukubali kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa fainali.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments