Michezo

Eti Ronaldo na Messi ndio wakali kwenye soka?? Eric CANTONA kasema hao wote sio, kataja jina la mkali wake !!

on

article-2455213-18B00C9F00000578-331_634x409

Hii story imesikika pia kwenye AMPLIFAYA jana April 15 2015, labda wewe hukusikia kile alichokisema staa wa soka wa zamani ambaye yuko kwenye vitabu vya kumbukumbu vya mastaa wa soka ambao dunia inawakumbuka kwa uzuri wao kwenye mchezo huo.

Ni kweli Cristiano Ronaldo amechukua tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo.. anaemfuatia kwa ukaribu zaidi ni Lionel Messi.. vijiweni kuna story bado kwamba nani bora kati yao.

Eric Cantona kataja jina tofauti.. YES.. ndio mawazo yake na yeye kwa hiyo usishangae akakutajia jina la staa wake.. amemtaja Javier Pastore staa mwingine wa soka raia wa Argentina, anachezea klabu ya Paris Saint-Germain.

.

Javier Pastore

Nimeangalia mechi mbili za PSG nikaona amavyocheza.. kwangu mimi yeye ni mchezaji mbunifu zaidi kwa sasa. Napenda jinsi Pastore anavyocheza“– Eric Cantona.

Nitafurahi kuona comment yako, unadhani ni sawa Cantona kumtaja Pastore kuwa ndio mchezaji kwa kumuangalia kwenye mechi mbili tu?

Tunaona mastaa kama akina Beckham wamestaafu wameamua kuwa wafanyabishara na wanamitindo, Cantona kwa sasa ni staa wa movie.

Cnatona FRONTT

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye FacebookTwitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments