Michezo

Capital One: Hiki ndicho Southampton walichoifanya Arsenal nyumbani kwao jana!

on

Arsenal walivubja rekodi ya miaka miwili kwenye Barclays Premier League jumamosi iliyopita kwa kukamilisha jumla ya pasi 741 katika ushindi wao wa magoli 3-0 dhidi Aston Villa.
Usiku wa jana katika uwanja wao wa Emirates ilikuwa zamu ya vijana wa Arsene Wenger kufundishwa soka na vijana wa Ronald Koeman Southampton.

Southampton ambao waliutawala mchezo wa jana kwa kiasi kikubwa walianza kwa kufungwa katika dakika ya 14 kwa goli zuri la adhabu ndogo nje kidogo na eneo la hatari la Southampton.
Saints wakasawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia Dusan Tadic.

Katika cha pili beki wa kulia wa kiingereza Nathaniel Clyne alifumua shuti kali la umbali yadi 39 lilomshinda golikipa mpya wa Arsenal David Ospina.

Na mpaka mpira unamalizika Arsenal 1-2 Southampton – na kwa Matokeo hayo Gunners wameyaaga mashindano ya Capital One.
Timu zilipangwa hivi:
Arsenal: Ospina 4; Bellerin 5 (Akpom 86), Chambers 6.5, Hayden 5, Coquelin 5; Rosicky 5, Diaby 5.5 (Cazorla 67); Campbell 5.5 (Oxlade-Chamberlain 71), Wilshere 5, Podolski 4; Sanchez 6.

Subs: Gibbs, Mertesacker, Martinez, Ajayi.

Booked: Rosicky, Wilshere

Manager – Arsene Wenger: 5

Southampton: Forster 6; Clyne 8, Fonte 7, Gardos 7.5, Targett 7 (Bertrand 85); Wanyama 6.5, Schneiderlin 9; Mane 7.5 (Long 72), Davis 7, Tadic 7.5; Pelle 7.

Subs: Davis, Cork, Mayuka, Reed, McCarthy.

Booked: Wanyama, Pelle, Tagett, Forster

Manager – Ronaldo Koeman: 8.

Referee: Keith Stroud.

IMG_7518.JPG

Tupia Comments