Michezo

Ratiba ya raundi ya 4 Capital 1 – Vigogo Man U, Chelsea, Arsenal, City kuumana na nani?

on

Baada ya mechi za raundi ya 3 ya michuano ya kombe la ligi maarufu kama Capital One kumalizika usiku huu, imetolewa ratiba ya hatua inayofauta ya michuano hiyo.

Manchester United baada ya kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Ipswich Town, sasa watacheza na  Middlesbrough nyumbani Old Trafford.

Arsenal baada ya kuiondoa Tottenham Hotspur sasa itacheza na Sheff Wednesday, wakati Liverpool au Carlisle watcheza dhidi ya Bournemouth – baada ya mchezo wa marudiano baina yao kutoa mshindi.

Chelsea watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Stoke City baada ya leo kuitoa Walsall kwa kuifunga 4-1.
Manchester City wataumana na Crystal Palace.

RATIBA NZIMA YA RAUNDI 4 CAPITAL ONE

Tupia Comments