Michezo

Matokeo ya mechi ya Sunderland Vs Man City yapo hapa pamoja na mechi nyingine za Capital One (+Pichaz&Video)

on

Klabu ya Manchester City usiku wa September 22 ilikaribishwa na klabu ya Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light kucheza mchezo wa Kombe la Capital One, mechi imemalizika kwa klabu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa goli 4-1.

2CA779E600000578-3245303-image-a-51_1442955206754

Manchester City ikiwa ugenini katika uwanja wa Stadium of Light imeibuka na ushindi wa magoli hayo kupitia kwa mchezaji wake wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero baada ya kupiga penati safi dakika ya 9 ya mchezo, goli la pili lilifungwa dakika ya 25 kupitia kwa Kevin De Bruyne baada ya kutumia vizuri pasi aliyoipata kutoka kwa Raheem Sterling.

_85693721_sterling_debruyne_afp

Goli la tatu Sunderland walijifunga baada ya Raheem Sterling kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi na kumgonga golikipa wa Sunderland Vito Mannone na kuingia nyavuni dakika ya 33. Wakiwa bado wanajiuliza nini kilichotokea Raheem Sterling dakika ya 36 akahitimisha idadi ya magoli 4, Sunderland baada ya kuonyesha jitihada ambazo ziliwasaidia kupata goli moja la kufutia machozi kupitia kwa Toivonen dakika ya 83 ya mchezo.

2CA6FEE000000578-0-image-a-19_1442953048978

Raheem-Sterling-scores-Ma-009

Matokeo ya mechi nyingine za Capital One zilizopigwa September 22

1

Hii ni video ya Magoli Sunderland Vs Man City

https://youtu.be/zePTH_YWx8s

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments