Stori Kubwa

EXCLUSIVE: Baada ya kurudi CloudsFM Gardner G. Habash kaongea haya matano.. aliwahi kutamani kurudi Clouds?

on

KIKUBWA ULICHOMIS CLOUDS UKIWA NJE:

Niliimis Clouds kama familia lakini pia nilimiss sana ile hali ya kuwa nafanya matamasha na Clouds kwa mfano tamasha kubwa kama la FIESTA ni tamasha ambalo lilitupeleka mikoa mingi sana, hiyo hali niliimis sana.

ULIWAHI KUTAMANI KURUDI CLOUDS?

Unajua yale matamanio mazuri yako kwa binadamu yeyote katika vitu mbalimbali alivyoviacha huko nyuma, tamanio langu kubwa ilikua ni pale nilipokua naona kuna sehemu ambayo Clouds wanapungukiwa ambayo kampuni yoyote duniani kuna sehemu wanapungukiwa na kwengine wanafanya vizuri, mimi nilipokua naona kama sehemu flani wamepungukiwa kidogo niliwaza ningekuwepo ningeshirikiana nao labda upungufu huu usingekuwepo japo hiyo haimaanishi kwamba mimi ni bora zaidi.

NI WAKATI GANI ULIPATA TAARIFA KWAMBA UNARUDI CLOUDS?

Mazungumzo yalivyoanza na mtu ambaye mimi namuita Wakala Shaffih Dauda mazungumzo yalianza tu kama mazungumzo ya kawaida kwasababu alivyonipa taarifa kwamba amekuwa mkuu mpya wa vipindi CloudsFM nikampongeza tu kikawaida, akaniuliza inawezekana vipi kufanya kazi pamoja na mimi, nikamwambia ni jambo linalowezekana na baada ya hapo ndio tukaanza mazungumzo na kufikishwa kwa viongozi, Jumapili April 3 2016 nikawa nimefikia makubaliano kamili nikaaga nilikokua nafanya kazi’

ULICHUKUA MUDA GANI KUFANYA MAAMUZI KWAMBA UNARUDI RASMI CLOUDS?

Nilipoongea na viongozi wa juu Clouds ndio nikasema kama hata Wakurugenzi wameona inafaa mimi kurudi kwenye familia na tushikamane pamoja kuendeleza hili gurudumu, nikaona sio vibaya kupokea wito wa watu ambao walinipokea tangu nilipoingia mara ya kwanza kwenye media wakanifundisha mengi nikakua na kutajwa kati ya wale bora, nikaona leo wananiita tena… ni nafasi ambayo sikuweza kuiacha

KITU GANI UNATAKA KIWAFIKIE MASHABIKI WA CLOUDSFM?

‘Msimu mpya wa CloudsFM ni tarehe 11 April 2016 na nitasikika moja kwa moja kupitia show ya JAHAZI na ndugu yangu Ephraim Kibonde, jingine la muhimu watu inabidi wajue ni haijalishi ni sehemu gani umepita ukaona kama umepunjwa, haijalishi ni kiasi gani umepoteza kile ambacho unakistahili… kumbuka tu Mungu ndie anayetoa na anaetoa bado yupo hivyo kama kuna kile unachostahili kupewa atakupa Mungu’

ULIIKOSA HII YA KIBONGO? MUME KAENDA KAZINI WIFE KALETA MCHEPUKO NYUMBANI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

ULIIKOSA YA RACHEL KUTANGAZA KUACHA BANGI NA KUMRUDIA MUNGU? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI..

Soma na hizi

Tupia Comments