Duniani

Mwanamke kapigwa faini na Askari, lakini bado akaongeza na ‘ASANTE’ yake juu…

on

Ni kawaida sana kutokea mtu amekosea kabisa barabarani akiwa anaendesha gari lake, trafiki akamkamata kwa kufanya kosa lakini bado mtu huyohuyo atalalamika kweli, kama ameonewa hivi !!

Umewahi kusema neno ‘ASANTE’ kwa mtu aliyekuadhibu kwa vile umefanya kosa? Mama wa Kimarekani amefanya hivyo kirahisi kabisa baada ya kukamatwa na Officer wa Police ndani ya Georgia, Marekani.

ford-police-interceptor-sedan

Mama huyo alikamatwa na Police kwa kosa la kuzidisha speed, akapigwa faini… lakini kwa kuonesha kwamba analitambua kosa lake, aliamua kuandika na barua kabisa kumshukuru Askari huyo kwa kumkamata kwa kosa hilo na kumpiga faini pia.

Bwana Officer, ni aibu yangu kwa kosa la kuzidisha spidi. Yako mengi mabaya yanazungumzwa na watu kuhusu Maafisa wa Polisi na kazi yenu ni hatari sana. Naomba utambue kwamba mimi pamoja na Familia yangu tunajiona wenye bahati kulindwa na watu wazuri kama nyie, ASANTENI SANA

Hii ndio picha ya Barua hiyo ambayo mwanamke huyo aliiandika kwa Polisi..

HT_alpharetta_public_safety_note_jt_150905_v4x3_16x9_992

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments