Mix

Chuo cha CBE wameyazungumza haya baada ya kuripotiwa kwa tuhuma za ufisadi chuoni hapo

on

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini kuhusu chuo hicho. 

Akizungumza na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema amesema tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa kutisha si za kweli na zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho…..

>>>“Chuo kinafanyiwa ukaguzi wa Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali na kwa kipindi cha miaka minne tumepata hati safi (clean audit report) kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 .” :- Prof. Mjema.

Prof. Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Ameongeza kuwa kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika. Mafanikio mengine ni kujenga hema kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya vipimo na mizani chuoni hapo.

ULIIKOSA HII YA WAZIRI WA ELIMU KWENDA MWENYEWE CHUO CHA MT. JOSEPH DSM BAADA YA KUPATA TAARIFA ZAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments