Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Gabriel Makalla amesema wakati Chama cha Mapinduzi kikiazimisha Miaka 48 tangu kiundwe kuna mafanikio mengi sana yamepatikana na lazima yasemwe watu wajue kuwa ilani imetekezwa kwa kiwango
Mfano Sekta ya Miundombinu imebadilika sana leo tunayo mpaka Reli ya kisasa, Umeme sasa unapatikana wa uhakika mpaka tunataka kuuza nje ,Sekta ya afya tunazahanati kama vituo vya Afya,Maji ndo usiseme hivyo tusherekee tukijua tumefanya kazi kweli.
Mwenezi Makalla amesema hayo akizundua sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM Mkoa wa Dar es salam
“CCM ni Chama chenye dhamana ya kuwaletea maendeleo hivyo tutaendea kuwaletea Ilani inayogusa wananchi kwa kuongeza mengi mazuri ndani yake .”
Aidha Makalla amezungumzia suala la wananchi na wanachama wote kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga pindi litakapofika Dar es salam kwani ushindi ni namba na CCM inataka kushinda mapema kila mtu amhimize mwenzake kwenda kujiandikisha.