Duniani

Ugonjwa wa cancer wamzidishia majonzi Celine Dion, baada ya kupoteza mume kafatia kaka yake..

on

Kwa muda mrefu huenda hujamsikia mkali wa muziki na mkongwe mwenye Tuzo na heshima nyingi duniani, Celine Dion… lakini kwenye vilivyokuwa vinaendelea nyuma ya pazia kwenye ukimya wake iko ishu ya kumuuguza mume wake na Manager wake, Rene Angelil ambaye kwa bahati mbaya amefariki siku chache zilizopita.

Celine na marehemu mume wake, Rene.

Celine na marehemu mume wake, Rene.

Wakati akiendelea na majonzi ya msiba huo, tatizo la cancer limegusa tena familia yake ambapo kaka yake, Daniel Dion naye amefariki kwa tatizo hilohilo la cancer akiwa nyumbani kwao Montreal Canada.

640_daniel_dion_celine_dion

Daniel Dion na Celine

Rene na Celine walifahamiana kitambo wakati Celine ana miaka 12, akafanya nae kazi kwa kipindi chote kama Manager wake na pia mume ambaye wamezaa watoto watatu.

Daniel amefariki akiwa na umri wa miaka 59 wakati Rene alikuwa na miaka 73.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments