Top Stories

Kama ulimis tamko la Chadema Kigoma

on

Chadema 1Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Kigoma Mjini kimetoa Matamko Matatu kuhusiana na hali ya kisiasa inayoendelea ndani ya chama hicho ambapo ajenda zilizochukua ukubwa ni ajenda ya tano kuhusu hali ya kisiasa ndani ya Chadema na ziara ya Dk.Slaa Mkoani Kigoma na ajenda ya sita ilikuwa taarifa ya mkutano mkuu.

Ajenda ya sita kuhusu hali ya kisiasa ndio ilivuta hisia za wajumbe ambapo mkutano mkuu umetoa tamko la kulaani vurugu alizofanyiwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Magharibi Shabani Mambo wakati wa kikao cha kamati kuu kilichowavua uwanachama Dk.Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba.

Mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo, mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kigoma Mjini Adam Shabani alisema baada ya majadiliano na wajumbe, mkutano mkuu umelaani vikali kitendo hicho.

Hiki ndicho alichokizungumza Mwenyekiti huyo wa Chadema wilaya ya Kigoma Mjini..

Tupia Comments