Habari za Mastaa

50 Cent anaenda tena Mahakamani, time hii anamshtaki mshauri wake kabisa!

on

Kwenye matukio makubwa ya 50 Cent mwaka huu hatuwezi kuacha kulitaja tukio la yeye kutangaza kufilisika… mengi sana yamesemwa juu ya kitendo hicho lakini mpaka sasa rapper 50 Cent bado anaendelea na kesi yake na mwisho wake wengi wetu hatujui ikakuwa lini!

Kwenye headlines zinazomhusu 50 Cent ipo na hii mpya niliyokutana nayo… 50 Cent anamshtaki aliyekuwa mshauri wake Andrew Jameson kwa madai ya kuwa jamaa huyo amekuwa akiingia mikataba ya chini chini kwa kutumia jina lake bila kumwambia wala kuomba ruhusa yake.

502

50 Cent.

Kesi hiyo ilipelekwa kwenye Mahakama ya Federal Bankruptcy Court, Connecticut siku ya jumanne ya tarehe 22 September na rapper huyo anadai fidia ya dola 810,000 ambayo kwa pesa ya sasa ya Tanzania tunaongelea kitu kama Bilion 1.6 na zaidi!

Mwanasheria wa Andrew Jameson ameongea na baadhi ya vyombo vya habari na kusema kuwa 50 Cent anadangaya na anataka aonekane mwema sana kwa watu haswa kwa kipindi hiki ambacho anajua Sheria haiwezi kumshambulia moja kwa moja, lakini hata yeye amekuwa akikwepa kumlipa mshauri huyo misharaha yake kwa miezi kadhaa sasa… kesi hiyo inategemewa kusikilizwa hivi karibuni.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments