Michezo

CEO Barbara wa Simba afikishwa Polisi

on

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuwa halijamfungulia kesi Polisi kiongozi yeyote wa soka.

Taarifa hiyo inakuja muda mchache baada ya afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez kufunguliwa kesi polisi na afisa wa TFF Jaqueline Kamwamu kwa madai ya kutolewa lugha isiyompendeza afisa huyo wa TFF baada ya kumzuia yeye na watoto kuingia eneo la VVIP uwanja wa Benjamin Mkapa December 11 2021 katika mchezo wa watani wa jadi Simba SC vs Yanga SC.

Inaelezwa kuwa kesi hiyo imefunguliwa katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Barbara inaelezwa alifika kituoni hapo January 20 2022 na kuwekwa ndani kwa saa kadhaa kisha kuachiwa.

Soma na hizi

Tupia Comments