AyoTV

VIDEO: Mbunge wa Ndanda Cecil Mwande kaguswa na mazingira magumu ya kujifungulia

on

Mei 9 2016 bunge la 11 limeendelea tene Dodoma  Katika kipindi cha maswali na majibu  Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe aliuliza…

>>‘Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga wodi ya Wazazi kwenye kituo cha Afya Chiwale kwa kuwa wazazi hujifungulia kwenye chumba ndani ya jingo ambalo hutumika kulaza wagonjwa wa kiume na kike?

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jafo anajibu…’Ni kweli kituo cha Afya Chiwale hakina wodi, Halmashauri imetenga shilingi milioni 80 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Chiwale

Ili kuharakisha utekelezaji wa mpango huo, Halmashauri imeshauriwa kutumia fursa ya mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya ili kupata mkopo utakaowezesha kujenga jengo la maabara na wodi ya kisasa ya wazazi kutokana na ukosefu wa miundombinu

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments