Top Stories

Baada ya abiria kulala njiani siku 2, maaskari wa JWTZ na JKT wafanya hili

on

Changamoto ya barabara inaendelea kuwatesa wakazi na wasafiri katika eneo la linalounganisha Wilaya ya Monduli na Karatu baada ya daraja lililokuwepo kuvunjika January 18, 2018 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Arusha.

Leo January 19, 2018 hali imezidi kuwa mbaya baada ya daraja la muda lililokuwa likitumika kuvunjika tena na kusababisha watu kukaa njiani kwa siku mbili bila usafiri hivyo kusababisha barabara kufungwa.

Ayo TV na millardayo.com zimefika eneo la tukio na kushuhudia askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ, na Jeshi la Kulinda Taifa JKT wakishirikiana na wananchi kujenga barabara ya muda ili kuwezesha magari na watu kuweza kupita huku wakisubri hatua zaidi za kurekebisha hali hiyo.

Uzinduzi wa mwongozo kwa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano

NGUO FUPI: “Jamani jamani… hatuwezi kutembea na futi mitaani” – TIBAIJUKA

Soma na hizi

Tupia Comments